ZIFAHAHMU NJIA ZAKUWA MZNGUMZAJI BORA
 Wapo baadhi ya wasomaji wangu walikuwa wakiniuliza "eti nifanye nini ili kuwa mzungumzaji mzuri mbele ya watu wengine? Swali hili kiukweli limekuwa likiwatatiza watu wengi sana kwa namna moja ama nyingine. Na kutokana na hali hiyo kumewafanya watu hao hao kuwa katika hali unyonge, kwani huisi watachekwa na sababu nyingine kama hizo. Lakini ukweli ni kwamba endapo utazijua siri hizi kuwa mzungumzaji bora zitakwenda kukusaidia kutoka katika hali uliyonayo hatimaye kuwa mzungumzaji mzuri . Zifuatazo ndizo mbinu kuwa mzungumaj bora: 1: Kuwa na taarifa za uhakika na kutosha. Moja ya njia bora ya kuwa mzungumzaji mzuri ni kuwa na utajiri wa vitu vingi katika kibubu cha ubongo wako . Watu wengi wanajiona hawawezi kuchangia maada yeyote ile mbele ya wengine hii ni kwa sababu wamekuwa hawana taarifa sahihi na za uhakika za kuweza kuzungumza. Hivyo Kama endapo nia yako ni kutaka kuzungumza mambo mbalimbali katika jamii yako ni lazima ujue vitu hivyo kwa undani zaidi. Kama u...