NJIA ZA KUMFANYA MTU AISHI KWA FURAHA DUNIANI

Watu wengi wanashindwa kuishi kwa na watu wengine kutokana na kutokujua mambo muhimu yafuatayo:;;;

1: Kuwa mkarimu kwa kila Mtu: kama utakuwa mkarima kwa kila kitu ulichonacho na kushirikiana na wengine utafanya upendwe na watu.

2: Kuwa na furaha muda wote hata pale watu wanapokuuzi:   hii itasababisha watu kutokujua kuwa wewe ni mtu wa aina gani tofauti na kuwaonyeshea kiburi.

3: Heshimu kila mtu hata kama ni adui yako:  kuwaheshimu watu wa rika zote ni njia ya kufanya uishi kwa furaha pasipo na mikwaruzo kwani kila mmja umemheshimu kulingana na nafasi yake.

4: Epuka kumdharau mtu  hata kama hana chochote,: wengi wanakuwa na dharau kutokana na pesa pengine walizo nazo  na hivyo kuwadharau wengine bila kujua maisha ni mzunguko

5: Kuwa mnyenyekevu kwa watu;: Endapo utakuwa  unajishusha kwa kila mtu  ambaye hata si rika lako utaonekana mtu  mwenye busara na utapendwa na watu.

Endapo utazingatia hayo utaishi maisha ya furaha yasiyo na chuki wala migogoro baina yako na watu.

By Mchome Agnes

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

HISTORIA YA MWANAMUZIKI KOFFI OLOMIDE

Koffi olomide