HABARI HAI
DC HAI AAGIZA WAWILI KUWEKWA RUMANDE BAADA YAKUIKOSESHA SERIKALI MAPATO.
Na Agnes's Mchome Hai
Mkuu wa Wilaya ya Hai Lengai Ole Sabaya ameuagiza uongozi wa shamba la mwekezaji la TUDLEY Estate LTD kulipa ndani ya siku saba deni la zaidi ya cha Shilingi milioni 700 ikiwa ni kodi ya serikali ya mkataba wa mauzo ya shea waliyokwepa wakati wa kubadilisha mmiliki wa shamba hilo kutoka kwa Konrad Legg kwenda kwa Trover Gifford.
Pamoja na agizo hilo pia mkuu huyo wa wilaya ameagiza Meneja na Mwanasheria wa Shamba hilo kuwekwa ndani saa 48 pamoja na kuchukuliwa hatua za kisheria wakipatikana na kosa la kumpotosha mwajiri wao na kumsababisha kukwepa kulipa kodi.
Hatua hiyo inakuja baada ya kubainika kuwa mwekezaji wa shamba hilo Konrad Legg aliingia mkataba na vyama vinne vya ushirika vya Mudio , Masama Roo , Sonu Ngira na Masama Sawe *MUROSOSANGA kwa kipindi cha miaka 35 kuanzia mwaka 1998 hadi 2025.
Sabaya amesema kuwa kutokana na mwekezaji wa kwanza kufanya mkabata wa mauzo bila kufuata sheria imesababisha serikali kukosa kiasi cha shilingi milioni zaidi ya milioni 700 zinazotokana na asilimia 20 za mauzo hayo.
Hata hivyo ameagiza Idara ya uhamiaji wilayani Hai kushikilia kwa muda hati ya kusafiria ya mwekezaji huyo raia ya Uingereza hadi pale atakapolipa Madeni hayo.
Maoni
Chapisha Maoni