Machapisho

Inaonyesha machapisho kuanzia Aprili, 2018

Ngoma safi kuivaa simba jumapil

Kikosi cha Yanga kinaendelea na mazoezi mjini Morogoro kujiandaa na mechi dhidi ya watani wao wa jadi Simba kwa ajili ya mchezo wa ligi utakaopigwa Uwanja wa Taifa, Jumapili ya wiki hii. Taarifa kutoka kambini zinaeleza kuwa wachezaji waliokuwa majeruhi, Ibrahim Ajibu pamoja na Andrew Vincent 'Dante' wanaendelea kuimarika kufuatia kuungana na wenzao juzi Jumatatu. Ukiachana na wawili hao, Donald Ngoma naye ameungana na kikosi cha Yanga mjini humo kujinoa kwa ajili ya mtanange huo wenye amsha-amsha kubwa katika soka la Tanzania. Ngoma ambaye alikuwa majeruhi kwa muda mrefu, hajakuwa na msimu mzuri kutokana na kuuguza majeraha yake, kitu ambacho kimesababisha akosekane dimbani. Aidha, Amis Tambwe naye ni mmoja wa wachezaji wanaojifua na Yanga kambini ili kujiweka sawa kwa ajili ya mechi ya Jumapili

Recordi alizoweka m salah ligi kuu england

Mchezo wa kwanza wa nusu fainali ya UEFA Champions League umechezwa katika uwanja wa Anfield jijini Liverpool kwa kuzikutanisha timu za Liverpool dhidi ya wageni wao AS Roma ya Italia.  Liverpool ambao hawajacheza hata ya nusu fainali ya UEFA Champions League toka 2008 wamefanikiwa kuanza vyema safari ya kuelekea fainali baada ya kufanikiwa kuifunga AS Roma kwa magoli 5-2, Mohamed Salah Roberto Firmino ndio wamehusika kuimaliza AS Roma.  Mohamed Salah amefanikiwa kufunga magoli mawili dakika ya 35 na 45 na kutoa pasi mbili za magoli kama ilivyokuwa kwa Roberto Firmino pia aliyefunga magoli mawili dakika ya 61 na 68 sambamba na kutoa pasi mbili za magoli huku Sadio Mane akifunga goli la tatu dakika ya 56.  Magoli ya AS Roma yalipatikana dakika za lala salama 81 kupitia kwa Eden Dzeko kabla ya dakika nne baadae Diego Perotti kufunga goli la pili kwa mkwaju wa penati, kwa matokeo hayo Roma katika mchezo wa marudiano watahitaji ushindi wa magoli 3-0 ili waitoe Liverpool wakati Li...

Mchezo wa simba na yanga kamera mua zafungwa

Yanga, Simba kamera 100 zafungwa Uwanja wa Taifa 19 hours ago  Dar es Salaam. Katika kuimarisha usalama kwenye Uwanja wa Taifa katika mchezo wa watani wa jadi kati ya Simba na Yanga Aprili 29, Shirikisho la soka nchini (TFF) , limetengaza kufungwa kwa kamera 109 uwanjani hapo. Afisa habari wa Shirikisho hilo, Clifford Ndimbo alisema watu wa usalama wamejipanga vyema kudhibiti vurugu zozote ambazo zinaweza kujitokeza katika mchezo huo

Ngorongoro heroes yarejea nchini

NGORONGORO HEREOS YAREJEA NCHINI 8 hours ago  Timu ya Taifa ya Vijana U20 (Ngorongoro Heroes) jana imerejea nchini ikitokea nchini DR Congo kwenye mchezo wake wa marudiano wa kufuzu fainali za Africa za Vijana U20 dhidi ya DR Congo. Wachezaji wa Ngorongoro ambao wamefanikiwa kuivusha timu hiyo kwenda raundi ya pili wamepewa mapumziko ya siku tatu kwa mujibu wa program ya Kocha Mkuu Ammy Ninje. Katika raundi ya pili Ngorongoro Heroes watacheza dhidi ya Mali mwezi ujao mchezo wa kwanza wakianzia nyumbani

Michezo leo

Club ya Dar es Salaam Young Africans ambayo ilikuwa inafindishwa na kocha George Lwandamina raia wa Zambia, sasa inajipanga kumtambulia kocha Mwinyi Zahera kama kocha wao mpya. Yanga itamtambulisha Mwinyi Zahera mwenye uraia wa nchi mbili za Congo DRC na Ufaransa muda wowote kama mbadala wa George Lwandamina aliyeamua kuondoka club hiyo kwa madai mbalimbali na kwenda kwao Zambia kujiunga na Zesco United .  Kocha Mwinyi Zahera atakayeanza kazi na Yanga hivi karibuni amewahi kuwa kocha wa vilabu kadhaa ikiwemo DC Motema Pembe ya kwao Congo DRC, AFC Tubize ya Ubelgiji na amewahi kuwa kocha msaidizi wa timu ya taifa ya Congo DRC.

Mbo yakumfanya mpenzi wako akupende zaidi

Mambo yatayomfanya mumeo akupende zaidi  Wapo baadhi ya wanawake hudiliki hata kutumia dumba hii yote ikiwa kuwafanya wanaume zao wawapende, lakini wengi wao wamesahau ya kwamba kufanya hivo sio chachu ya kufanya mahusiano hayo yakue bali ni kuyadidimiza. Lakini ukweli kwamba mambo ya libwata yamepitwa na wakati katika karne hii hivyo ili mumeo akupende zaidi katika mahusiano yenu unatakiwa kufanya yafautayo; 1. Muamini mmeo au mchumba wako. 2. Usimkatishe tamaa katika maono yake. 3. Usimlazimishe kupenda mambo unayoyapenda. 4. Kila wakati kila unapo tatizo ni vyema ukamwambia kuliko kusema kwa wengine. 5. Usidhani kwamba hawezi kutambua uwepo na uzuri wa wanawake wengine hivyo mfanye awe karibu nawe ilia one thamani yaw ewe pekeee.. 6. Usilazimishe kuwajibika juu ya mambo yako: Kama vile kwenda saluni, umeme, vocha na mambo mengine hasa kama bado mko katika mchakato wa uchumba, kama atafanya hivyo mwache afanye mwenyewe msimlazimishe eti kwa sababu shosti wako huwa an...