N atumaini kuwa si mgeni sana na jina hili la Kofii Olomide hususani kwa kile kizazi cha 2000's kushuka chini na hasa hasa wale vijana wazamani kwenye miaka 1990's. Koffi Olomide ni msanii mkubwa wa muziki wa Dance wengi upenda kuuita "Lingala" kutoka huko nchi ya Demokrasia ya Congo. Jina kamili la mwana'lingala huyu ni Antoine Christophe Agbepa Mumba, maarufu kama Koffi Olomide alizaliwa miaka 58 iliyopita (Julai 13, 1956) siku ya Ijumaa huko Kisangani Demokrasia ya Congo. Jina hilo la Koffi alipewa na mama yake mzazi akiwa na maana ya kuzaliwa kwake siku hiyo ya ijumaa (Friday). Koffi amezaliwa na kukulia kwenye familia ya hali ya kawaida ikiwa na maana kwamba familia yao haikuwa ya juu kiuwezo wa ya chini (middle class - Family) Alianza kujifunza kuimba na kuandika mashairi akiwa na umri mdogo na kuwashangaza majirani zake hususani umahiri wake wa kutunga mashairi na kupiga gita. ELIMU: Koffi aliweza kubainika na baadhi ya wanafunzi wenzie na walimu wake ...
Maoni
Chapisha Maoni