MADHARA YA MAGONJWA YA KINYWA KWA WENYE VVU
WANAYOPASWA KUFANYA WENYE VVU KUEPUKA MARADHI YA KINYWA Watu wengi walioathiriwa na virusi vya ukimwi (VVU), hupatwa na maradhi tofauti ya kinywa. Na wakati mwingine wanapopatiwa matibabu ya kinywa na madaktari, huwa hawasemi kutokana na sababu mbalimbali ikiwemo ya usiri wa mgonjwa kwa daktari kuhusu afya yake kwa ujumla, kukosa umakini kwa daktari ama sababu nyingine yoyote. Hivyo, kushindwa kutambua hali hii, husababisha mhusika kukosa matibabu sahihi, hivyo kuendelea kuumia. Kwa maana hiyo, ni muhimu kwa waathirika kufahamu ya kwamba, wanapokwenda kwa daktari wa kinywa na meno kupatiwa tiba, ni vyema wakaelezea historia nzima ya afya zao. Hii itamsaidia daktari kupata ufahamu wa kutosha na kumuwezesha kutoa matibabu husika na kikamilifu. Kwani baadhi ya maradhi yanayoweza kumkumba muathirika wa ukimwi kinywani ni pamoja na kinywa kuwa kikavu (Xerostomia), fangasi (candidiasis), maradhi ya fizi (Periodontal diseases), saratani ya kinywa na vidonda kinywani. Ila izingatiwe ma...