Machapisho

Inaonyesha machapisho kuanzia Mei, 2018

Siri ya kudumu katika mahusiano ya ndoa

Zipo changamoto ambazo zinazosababisha ndoa nyingi kufa. Hata hivyo kufa kwa ndoa hizo husababishwa na vitu vidogovidogo ambavyo watu wengi wamekuwa hawavitilii maanani. Hata hivyo siku ya leo nimeona ni vyema nikujuze siri ya kudumu katika mahusiano ya ndoa. Je ni vitu gani? Twende sawa: 1. Mapenzi ya kweli. Ili uweze kudumu katika ndoa yako ni lazima uwe na mapenzi ya kweli kwa mwezi wako. Upendo wa kweli mara kadhaa huwa haupimwi kwa maneno tu bali ni kwa vitendo. Hivyo katika kuhakikisha unafurahia maisha ya mahusiano hakikisha unajua ni kipi kitokachomfanya mpenzi wako ajue ya kwamba unampenda. Hilo ni suala la msingi ambalo ni vyema ukalijua. 2. Uvumilivu. Kitu ambacho pia kitakusaidia kuweza kukaa kwa muda katika ndoa yako ni kuhakikisha unalijua lile somo la uvumilivu. Kama ambavyo siku ya ndoa yenu mliampa ya kwamba mtadumu katika ndoa yenu katika shida na laha. Hivyo ili kuweza kulitimiza hilo ni lazima ukumbuke kiapo chenu. Hii itawasidia sana kuweza kutengeneza maelewan...